September 28, 2020

Mjue Shangazi Masika pamoja na maoni yake kuhusu mila na tamaduni za wapwani

Shangazi ni Cultural Ambassador wa kujitolea. Shangazi ni mshairi, mwandishi wa riwaya na ni mtoa mawaidha.

Wengi wetu tunakufahamu kama Shangazi Masika, hebu tuambie jina lako halisi

Jina langu halisi ni Constance Masika Beja

 

Unafanya kazi gani?

Mimi ni mwanabiashara. Pia nashughulika na events tofauti tofauti kama vile harusi, fashion shows na mentorship programmes kwa mashule na kwa jamii kwa jumla, ambazo ni za charity

 

Ulizaliwa wapi, na ni mzaliwa wa ngapi?

Nilizaliwa Kongowea baadaye tukaenda Kaloleni ambako ndiko “mudzini” kabisa. Mimi ni mzaliwa wa tano kwa familia ya watoto sita tukiwa wasichana watatu na wavulana watatu

 

 Je wazazi wako wako hai? Na je wanafanya kazi gani?

Babangu alifariki miaka mitano nyuma. Mara nyingi ukinikumbusha kifo chake nahisi machozi yanitiririka kwani aliaga ghafla. Alianguka akiwa kwenye zizi la ng’ombe akikamua maziwa na hakuongea tena hadi siku ya pili mchana, akakata roho. Inaniuma sana kwani sikuwahi muona babangu siku ya mwisho ya uhai wake kwani nilikuwa kazini South Coast. Alimuacha mamangu ambaye amekuwa mwanabiashara siku nyingi ila kwa sasa hushughulika na kazi zake kiasi za shambani.

shangazi masika

Shangazi Masika ni nani hasa?

Mwanzo wacha nieleze mbona nailijiita Shangazi. Waduruma huzaa mashangazi, nami hii fani nimeiboresha wakati babangu alipofariki maana yeye alipenda kuniita Shangazi kwa kuwa wale dada zangu ni mama zake. Hivyo nikaona kumuenzi ni bora nitumie Shangazi Masika. Watu wakiniita, kwa mbali naisikia sauti ya babangu kipenzi Charles Tim.

Shangazi ni Cultural Ambassador wa kujitolea. Shangazi ni mshairi, mwandishi wa riwaya na ni mtoa mawaidha.

 

Ulisomea wapi?

Nilisomea St. Michaels Primary, kisha  baadaye nikajiunga na shule ya upili ya Sokoke. Baada ya hapo nikajiunga na Jara College of IT, na kisha Karen International College ambako nilisomea Sales and Marketing. Nimefanya pia Short Courses za Ukulima kupitia kampuni niliyokua nikifanya kazi.

 

Shuleni ulijihusisha na michezo ama activities gani?

Nilikuwa mwanaskauti ambayo nimekuwa Commander toka darasa la sita hadi nane. Nikawa kwa kundi la PAS (Presidential Award Scheme) hadi nikapata Gold Medal yangu mlima Longonot. Michezoni nilikuwa nacheza volleyball tena captain, na pia nilicheza basketball, forward position. Ninacheza basketball hadi leo, na mimi ni mpenzi wa mazoezi sana.

 

Wakati ukisoma ulikua na ndoto za kuwa nini ama kufanya kazi gani baadaye?

Nilitaka sana kufanya Communication ama kuwa Mwanajeshi

 

Ulianza lini kupenda na kujihusisha na utamaduni?

Utamaduni kwa kweli niliupenda toka niko mdogo kwani nimekuwa na jukumu la kumpokea askofu akihudhuria sherehe za kanisani kwetu Giriama Parish; kisha nikaja kujitoa kimasomaso mimi mwenyewe kuanzia 2015.

 

Ni nini kilikuvutia katika mambo ya utamaduni?

Mwanzo kabisa utamaduni hufanya mtu akajitambua chimbuko lake. Kama mie SHANGAZI watu waikiniona husema ni mjaluo, labda kwa rangi niliyo nayo. Ila mimi Mduruma-Mtaita na nimelelewa kwa Wagiriama, sasa kuupenda utamaduni kwanipa identity.

Pili, utamaduni wanifanya naweza kuwafikia walio chini kimaisha na wakafunguka bila hofu.

Tatu, utamaduni nimeupenda kwa sababu nafanya mashairi kimijikenda sasa siwezi tumia profile ya western culture.

shangazi masika

 

Je kwa maoni yako, unafikiri wapwani wamezipuuza mila na desturi zao? Na je unaona ni kwa nini?

Wapwani kwa asilimia kubwa wamezipuuza ama kutupilia mbali mila na desturi zao, jambo ambalo linanitia hofu kuona utamaduni wetu ukididimia.

Kinachopelekea mila kutupiliwa ni maisha ya kileo. Watu wanaiga sana wazungu, na pia dini na makanisa yanayoenea kwa kasi ya kuzidi moto wa kichaka kikavu na kila mhubiri kuingia na sheria zake kulingana na wanavyoitafsiri bibilia

 

Kuna umuhimu gani wapwani kuzishabikia na kujivunia mila na tamaduni zao?

Mila ni kitambulisho chetu, na pia mila zina muongozo wake. Hivyo watu niwazipime zile mila elekezi na wazishikilie. Kwa mfano, mila ya kusindikwa kwa mume kama umepata ujauzito yasaidia wavulana kuchukua majukumu, hivyo huleta uoga wa kulifanya tendo hilo kiholela. Pia yasaidia msichana asiwe single, kupelekea kudharauliwa na jamii.

 

Ni vitu gani unavyovifanya kibinafsi ili kuhamasisha wapwani juu ya umuhimu wa tamaduni?

Ninafanya charity na mentorship programmes kwa jamii kupitia kampuni yangu Kikwetu Kiafrika, ambapo mimi ndio Executive Director

 

Ni changamoto zipi unazoipitia katika kazi yako?

Changamoto zipo japo siwezi sema ni nyingi za kunivunja moyo. Kwa mfano:

  1. Kukosa ufadhili kwa event.
  2. Mtu kucancel order na labda alikuwa amekuita kwenye harusi.
  3. Watu kubaki na vifaa vya kazi yangu ya utamaduni.

 

Unakariri mashairi ya Kigiryama. Je unayaandika mwenyewe au kuna mtu hukuandikia?

Mashairi nayatunga mwenyewe na sifanyi ya kigiryama tu; niko nayo ya kiswahili na kimombo

 

 

Uligundua lini kwamba unayo talanta ya mashairi?

Toka nipo darasa la sita

 

Mashairi yako huzungumzia nini hasa?

Mashairi yangu huzungumzia maadili. Mengine huzungumzia mapenzi na pia nasaha.

 

Ni mambo gani zaidi unayojihusisha nayo?

Najihusisha na mambo ya fashion and design; hata nataka kurudi chuo kwa hilo

 

Ushawahi kupata tuzo yoyote au kutambuliwa na viongozi kwa juhudi zako unazozifanya?

Ndio, tuzo nimezipata, na mara nyingi huwa kwa mfumo wa pesa. Nafahamu viongozi wanitambua maana kama kwa mkutano kiongozi anaweza akaulizia Shangazi, hiyo ni credit.

 

Na ni kipi ambacho pengine watu wengi hawakijui kukuhusu?

  • Watu hawafahamu kuwa mimi nina vidole sita, hahahaaa! Japo vile vya sita nilifanyiwa surgery, ila ukishika kiganja changu utaona.
  • Shangazi ni mtu asiependa aibu na vurugu.
  • Shangazi hupenda kuongea ukweli

 

Ungekutana na Rais Uhuru Kenyatta leo, unemwambia nini?

Ningemuomba aweke sheria kuwe na Cultural Day ya Kenya nzima kama vile kunayo Jamhuri ama  Mashujaa Day ili watu waweze kuadhimisha tamaduni zao. Pia kwa Wamijikenda ningemuomba awajengee Cultural Centers ambazo hazina sheria nyingi kama KAYA ili watu waendeleze talanta zao, ziwe ni za kuimba ama utengenezaji viombo vya aina aina.

 

Una maono yapi kwa kipindi cha miaka 3-5 ijayo?

Nina maono ya kuwa na Mijikenda Academy ambazo hizo ni centres za kusoma kikwetu. Kunayo maono mengi ambayo wacha kwa sasa nibaki nayo moyoni.

 

Unawashauri nini vijana wa pwani?

Mwanzo wapende utamaduni wetu ili kujua chimbuko lao, na pia wajitahidi sana kuijua lugha ya Mijikenda angalau.

 

Wito wako kwa jamii ni upi?

Wito wangu kwa mradi wangu wa kijamii watu wajitolee wapate kutoa kupitia KIKWETU KIAFRIKA ambayo tunafocus kwa maboma yaliyo jirani na KAYA ili kuwahamasisha wasiwe wanapora mali ya Kaya, kwa mfano kukata miti. Hivyo tutasaidiana hata kupanda miti ili kutunza misitu yetu.

Related articles